Chelsea yaiadhibu Spurs, yatinga fainali

Hot Michezo

Chelsea imetinga fainali ya Kombe la Ligi baada ya uisambaratisha Totenham Hotspurs kwa mikwaju ya penati.

Wababe hao wa Daraja la Stanford waliingia uwanjani wakiwa nyuma kwa goli walilonyukwa kwenye mchezo wa wanza.

Shukurani za pekee zimuendee N’Golo Kante aliyefunga dakika ya 27 kabla ya Eden Hazard kupigilia msumari mwingine dakika ya 38 ya mchezo.

Lorrente aliinua shangwe kwa mashabiki wa Spurs baada ya kuipatia timu yake goli dakika ya 50 ya mchezo na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-2.

Mpaka dakika 90 zinakwisha matokeo ya jumla yalikuwa yalikuwa 2-2.
Willian, Cesar Azpilicueta, Jorginho na David Luiz waliweka wavuni mikwaju yao ya penati huku Eric Dier na Lucas Moura wakipoteza penati zao hivyo kufanya Chelsea kusonga mbele baada ya kushinda kwa penati 4-2.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *