Simba yatinga Robo Fainali Mabingwa Afrika

Hot Michezo

Dar es Salaam, TANZANIA.

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kuingia robo fainali ya klabu bingwa Afrika baada ya kuifunga AS Vita kutoka Kongo kwa magoli 2-1.

AS Vita ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Kasengu.

Dakika ya 36 ya mchezo, Mohamed Husein aliisawazishia Simba goli na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare.

Kipindi cha pili kilianza kwa kupooza huku kila timu ikifanya mashambulizi ya kushtukiza kabla ya Chama (pichani) kuipatia Simba bao la pili dakika ya 90 ya mchezo.

Kwa ushindi huo wa 2-1, Simba imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ikiwa na alama 9 nyuma ya Al Ahly inayoongoza kundi lao la D ikiwa na alama 10.

JS Saoula inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 8 na AS Vita inashika nafasi ya nne na ya mwisho ikiwa na alama 7.

Timu nane zilizoingia hatua ya robo fainali ni Al Ahly, Simba, Esperance, CS Constantine, TP Mazembe, Horoya, Mamelodi Sundowns na Wydad Athletic.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *