Moto wateketeza kanisa la Notre-Dame cathedral Ufaransa, simanzi yatawala

Habari Hot

Paris, UFARANSA.

Imekuwa siku ya nzito na ya huzuni kubwa, hakuna aliyeamini macho yake!

Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya hapo jana jumatatu moto mkubwa kuzuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame jijini Paris Ufaransa ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka.

Vikosi vya zima moto vinaendelea kuzima moto huo katika kanisa hilo lililodumu kwa takriban miaka 850.

Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na mto huo huku moto katika minara miwili ya kengele umefanikiwa kuzimwa.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini maafisa wanauhusisha mkasa huo na shughuli ya ukarabati inayoendelea.

Wazima moto wanafanya kila juhudi kuokoa vito vya thamani vilivyoko ndani kanisa hilo na pia kuzuia mnara wa upande wa kaskazini kutoporomoka.

Maelfu ya watu wamekusanyika katika barabara zilizo karibu na kanisa hilo kushuhudia mkasa huo wakiwa kimya.

Baadhi yao walionekana wakidondokwa na machozi, huku wengine wakiimba nyimbo za sifa na kuomomba Mungu.

Makanisa kadhaa nchini Ufarasa yamekuwa yakipiga kengele kuashiria uharibifu wa moto huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alifika katika eneo la tukio amesema mawazo yake yako na waumini wote wa kanisa katoliki na wafaransa wote kwa ujumla.

“Sawa na watu wengine nchini, nimesikitika sana kuona sehemu ya maisha yetu ya kila siku ikiteketea.”

Macron awali alifutilia mbali hutuba muhimu kwa taifa kufuatia moto huo, alisema afisa wa Élysée Palace.

Msemaji wa kanisa hilo pia amekiri kuwa sehemu kubwa imeteketea na bado inaendelea kuteketea.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *