Familia ya Wanyama kumshuhudia akikipiga na Liverpool kwenye fainali ya UEFA

Hot Michezo

Nairobi, KENYA. Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, na kiungo wa timu ya Tottenham, Victor Wanyama ataisafirisha familia yake kwenda kumshuhudia akicheza kwa mara ya kwanza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi hii.

Pambano hilo la fainali linatarajiwa kupigw akatika dimba la Wanda Metropolitano, mjini Madrid ambapo Tottenham Hotspurs anayoichezea Wanyama itakuwa na kibarua kizito mbele ya Liverpool katika mchezo huo wa fainali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ndani vimeeleza kuwa Wanyama ameiambia klabu yake kuwa ataalika watu sita wa familia yake inayotarajiw akusafiri hii leo.

Wanyama atalazimika kutumia zaidi milioni 2 za Kenya kwa ajili ya kusafirisha watu sita katika familia yake, akiwemo mama yake.

Hii siyo mara ya kwanza kwa mchezaji kutoka kwenye familia ya Wanyama kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuwa kwa Victor itakuwa mara yake ya kwanza.

Kwani itakumbukwa kuwa Kaka wa Victor, Macdonald Mariga akiwa na Inter Milan aliyekuwa mchezaji wa kwanza kutoka kwenye familia hiyo, kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa mwaka 2011/12.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *