Aliyeua wagonjwa 85 ahukumiwa kifungo cha maisha

Habari Hot

Berlin, UJERUMANI. Muuwaji na ambaye alikuwa muuguzi wa zamani Niels Hoegel amehukumiwa jana kifungo cha maisha kwa kuwauwa wagonjwa 85.

Jaji Sebastian Buermann alimwambia mtu huyo aliyehukumiwa kuwa kosa lako haliwezi kufikirika. Jaji huyo aliongeza kwamba nahisi kama vile wewe ni mhasibu wa kifo, na pengine fikira mbaya zaidi haziwezi kuelezea ukweli wenyewe.

Hoegel hapo kabla alishitakiwa kwa kuwauwa wagonjwa 100 wakati akiwa kazini kama muuguzi kuanzia Juni 1999 hadi 2005.

Wahanga, wakiwa ni watu wa rika tofauti na tabaka mbali mbali, wengine wakiwa katika hali mbaya kiafya na wengine wakiwa katika hatua za kupona, walitoa matumaini yao katika kituo hicho cha afya katika jimbo la Lower Saxony ambako Hoegel alikuwa akifanya kazi.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *