Guinea, Madagascar zatoshana nguvu AFCON 2019

Hot Michezo

Cairo, MISRI.

Timu ya taifa ya Guinea jana ilitoshana nguvu na Madagascar kwenye mchezo wa raundi ya kwanza wa kundi B kwenye kinyang’anyiro cha kombe la mataifa ya Afrika.

Guinea yenye historia nzuri ya kucheza michuano hiyo, ilipewa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Madagascar ambayo haina historia ya kushiriki mara kwa mara mashindano hayo.

Magoli ya Guinea yamefungwa na Kabba (34′) na Kamano (66′) kwa mkwaju wa penati huku magoli ya Madagascar yakiwekwa kambani na Anicet (49′) na Carolus (55′).

Kwa sare hiyo, kundi B linaongozwa na Nigeria huku nafasi ya pili ikienda kwa Guinea. Madagascar inashika nafasi ya tatu huku Burindi ikiwa ya mwisho.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *