Rais wa FIFA ateta na Rais wa Madagascar, Ikulu ya Antananarivo

Hot Michezo

ANTANANARIVO, MADAGASCAR

RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino, jana Jumatatu jioni, amekutana na Raisi wa Madagascar, Andry Rajoelina katika Ikulu ya nchi hiyo, kwa maongezi kuhusu maendeleo ya soka ya kisiwa hicho kilicho kwenye Bahari ya Hindi.

Infantino ameisifu Madagascar kwa mapinduzi ya soka, aliyosema yanachangiwa na sera bora za michezo za Serikali ya Rajoelina katika kuhakikisha mchezo huo unakua na kuendelea vyema ndani ya taifa hilo.

Rais wa FIFA, GIanni Infantino kushoto, akimkabidhi jezi Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, alipomtembelea Ikulu ya Antananarivo jana Jumatatu jioni.

Madagascar wanamiliki moja ya vituo bora vya soka Afrika katika kukuza na kuendeleza soka la vijana. Nchi hiyo ilifanikiwa kutinga hatua ya 16 ya fainali zilizopita za Mataifa ya Afrika (AFCON 2019), zilizofanyika nchini Misri.

Ni mafanikio yaliyoiingiza nchi hiyo katika orodha ya mataifa matano bora ya Afrika yanayowania Tuzo ya Timu Bora ya Mwaka ya Afrika kwa Wanaume, inakochuana na Algeria, Nigeria, Senegal na Tunisia.

Mshindi wa kategori hiyo na wengine saba wa Tuzo za Ubora za CAF, watatangazwa katika ‘usiku wa tuzo,’ hafla itakayofanyika Jumanne ya Januari 7, 2020, huko Hurghada, nchini Misri.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *