Mchungaji Msigwa atetea Uenyekiti Kanda ya Nyasa Chadema

Hot Siasa

MBEYA, TANZANIA

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, ameibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kuwania Uenyekiti wa Kanda ya Nyasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa Kibo jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi huo, Ezekiel Wenje, Mchungaji Msigwa ambaye ametetea nafasi hiyo, ameshinda kinyang’anyiro hicho kwa kupata 66 (sawa na asilimia 62.3), akiwashinda Boniface Mwabukusi aliyepata kura 26 (sawa ana asilimia 24.5) na Sadrick Malila – kura 14 (sawa na asilimia 13.2).

Katika taarifa yake wakati akitangaza matokeo, Wenje alisema jumla ya wapiga kura waliokuwa wamejisajili kwa ajili ya uchaguzi huo ni 108, waliopiga kura walikuwa 106, huku mbili zikiharibika.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *