Mshindi Ballon d’Or 2019 kujulikana leo, Ronaldo kukacha tena hafla ya tuzo?

Hot Michezo

PARIS, UFARANSA

TUZO ya Mchezaji Bora ya Ballon d’Or 2019 inatolewa leo usiku nchini Ufaransa, wakali watatu wakitarajia kuchuana katika uteuzi wa mwisho, lakini maswali ni mengi, yakiwemo je Cristiano Ronaldo atahudhuria hafla hiyo? Je nani atatwaa tuzo hiyo?

Ronaldo aliikacha hafla ya kukabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA, ambayo ilitwaliwa na beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk, anayetambulika pia kwa jina la VVD. Mholanzi huyo na Lionel Messi ndio waliohudhuria, Ronaldo akaikacha hafla.

Joto kuelekea usiku wa tuzo limezidi kupanda, huku kila mmoja akijaribu kumpigia chapuo nyota anayeamini anastahil kutwaa tuzo hiyo kubwa zaidi ya ubora miongoni mwa wanasoka duniani, lakini wanaowapigia debe mahasimu Messi na Ronaldo ni wengi sana.

Hapa chini kuna takwimu fupi za mafanikio ya uwanjani ngazi ya klabu kwa wakali hao watatu walioingia fainali, ambapo mmoja wao anaweza kutawazwa mshindi leo.

Lionel Messi vs Cristiano Ronaldo ngazi ya klabu 2019

MESSI

Mechi 44

Mabao 41

Assists 15

RONALDO

Mechi 35

Mabao 20

Assists 4

Mabao ndani ya Ligi Kuu tano bora Ulaya 2019

Robert Lewandowski 45

Lionel Messi 41

Karim Benzema 33

Kylian Mbappe 33

Sergio Aguero 32

Virgil Van Dijk 2019

Tackles

Alishinda 75.6 %

Alipoteza 24.4 %

Mipira ya juu (Aerials Duels)

Alishinda 75.4 %

Alipoteza 24.6 %

Mabao na Assists za mabeki wa kati

Virgil Van Dijk 11

Fabian Schar 6

Callum Chambers 6

David Luiz 5

Kurt Zouma 5

Hii ni kwa mujibu wa Goal.com

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *