Sumaye: Nang’atuka Chadema, sijiungi na chama chochote

Hot Siasa

ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Frederick Sumaye, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho leo, huku akisema ‘hajanunuliwa’ na wala hajiungi na chama chochote cha siasa.

Sumaye ameyasema hayo asubuhi hii alipozungumza na vyombo vya habari, akisisitiza kuwa uamuzi wake hautokani na kinachoweza kuitwa ‘kununuliwa’ na vyama kama ACT-Wazalendo au CCM, bali kwa kile alichokiita kufifishwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.

“Najiondoa Chadema kwa kutumia ibara ya 5, kifungu kidogo cha 4 (1). Sihamii chama chochote cha siasa, ingawa najua mengi yatasemwa, lakini niwaambie kuwa, kama nilinunuliwa wakati najiunga Chadema, basi huenda ikawa hivyo wakati huu napojiondoa.

“Wanaweza kusema nimenunuliwa ACT-Wazalendo au CCM, lakini ukweli ni kwamba nimetathmini na kugundua demokrasia ndani ya chama haifuatwi na hivyo sitotendewa haki katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, ambao ndio ulioniibulia chuki zote,” alisema.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *