Pambalu Mwenyekiti mpya Bavicha, ngoma ilikuwa ngumu usipime!

Hot Siasa

DAR ES SALAAM, TANZANIA

ZIMETUMIKA siku mbili kukamilisha mchakato mgumu na wa aina yake wa kupata viongozi wa Baraza Kuu la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), tafsiri inayomaanisha kwamba ilikuwa ngoma nzito.

Juzi, baraza hilo lilianza mchakato wake wa uchaguzi wa viongozi, ambao ulikuja kukamilkka jana jioni na kupata viongozi wa baraza, hii ni baada ya uchaguzi huo kurudiwa kufanyika mara mbili kutokana na wagombea waliokuwa wakiwania nafasi kushindwa kuvuka asilimia 50 ya kura.

Katika uchaguzi huo, John Pambalu aliibuka kidedea katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bavicha Bara, akipata kura 150, huku Moza Mushi akiibuka Makamu Mwenyekiti Bara kwa kura 134.

Utaka kujua zaidi kuhusu mchakato mzima na matokeo, pata nakala ya gazeti la TanzaniaDaima leo Jumatano Desemba 11

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *