AHUKUMIWA kifungo cha maisha jela kwa kubaka mtoto wa miaka mitatu

Hot Kitaifa

BUNDA, TANZANIA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imemuhukumu kifungo cha maisha jela, Masatu Mjarifu (35), ambaye ni Mvuvi na mkazi wa Kijiji cha Mahyolo wilayani humo, baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.

Hukumu hiyo ilitolewa jana naa Hakimu Mkazi Mwandamzi wa Mahakama hiyo, Jackline Rugemalira, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka, pasipo kuacha shaka yoyote.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Inspekta wa Polisi Theophil Mazuge, alisema kuwa Desemba 26 mwaka 2018, saa 2 asubuhi, mshitakiwa huyo alikwenda nyumbani kwa jirani yake na kumchukua mtoto huyo na kuingia naye chumbani kwake kisha kumbaka.

Habari zaidi juu ya tukio hilo na hukumu yake, ikiwemo namna mbakaji alivyojarbu kutoroka na kukamatwa, pata nakala ya gazeti la TanzaniaDaima leo Alhamisi Januari 9

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *