UBAKAJI; Mtoto wa miaka 10 anajisiwa, auawa na mwili wake kutelekezwa msituni

Hot Kitaifa

KATAVI, TANZANIA

KIZA kinene cha mauaji na matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kimeendelea kuufunika mwaka mpyaa wa 2020, hii ni baada muendelezo wa kuripotiwa kwa matukio, kunajisiwa na kuuawa kwa mwanafuzni wa darasa la nne, Shule ya Msingi Katisunga, Mpanda mkoani Katavi.

Taarifa za tukio hilo zinapasha kuwa, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 10 (jina linahifadhiwa), ameauawa kikatili na mwili wake kutupwa vichakani, baada ya kunajisiwa na watu wasiojulikana.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo alikumbwa na kadhia hiyo majira ya saa 5 asubuhi jana, katika msitu wa Katisunga, wakati akitoka kisimani kuteka maji akiwa na rafiki yake. Kamanda wa Polisi Katavi, Benjamine Kazuga, amethibitsha kutokea kwa tukio hilo.

Habari hii iko kwa kina ndani ya gazeti la TanzaniaDaima leo Ijumaa Januari 10, pata nakala yako tafadhali.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *