Mourinho: Tottenham imestahili ushindi, lakini Southampton haikupaswa kupoteza…

Hot Michezo

LONDON, UINGEREZA

MRENO mwenye maneno mengi, Jose Mourinho, amesisitiza kuwa kikosi chake cha Tottenham kimestahili ushindi wa mbinde wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton, katika mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA, iliyochezwa Jumatano usiku, lakini akasema timu bora imepoteza ndani ya uwanja.

Spurs ililazimika kupambana kutoka nyuma kwa mabao 2-1 hadi dakika 18 kabla ya filimbi ya mwisho, kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London, baada ya mabao ya Shane Long na Danny Ings yaliyokuja baada ya Jack Stephens kujifunga.

Hata hivyo, Lucas Moura amafunga bao la kusawazisha kwa kutoka yadi 18, kisha rafu ya kipa wa Southampton, Angus Gunn, ikazaa mkwaju wa penalti iliyowekwa kimiani na Son Heung-min dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi.

Kwa matokeo hayo, Tottenham sasa itaumana na Norwich City katika raundi ijayo ya michuano hiyo, lakini Mourinho akakiri kuwa wapinzani walikuwa bora licha ya kupoteza, na kwamba Spurs wamestahili ushindi licha ya kutokuwa bora mchezoni.

“Nimekuwa mkweli na niseme wazi kwamba timu bora imepoteza ndani ya uwanja, lakini timu yamngu imestahili kushinda., kwa sababu haikujiwekea ukomo wa upambanaji kuweza kupata matokeo,” alisema kuiambia BT Sport.

Livescore.com

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *