AJALI, uzazi pingamizi vyatajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya kifafa

Habari Hot

DAR ES SALAAM, TANZANIA

AJALI, uzazi pingamizi na minyoo, vimetajwa kuwa ni mojawapo ya vyanzo vya ugonjwa wa kifafa.

Aidha ugonjwa huo huwapata zaidi vijana wenye umri wa wastani wa miaka 15, huku asilimia 75 ya wanaougua ugonjwa wakiamini tiba ipo kwa waganga wa kienyeji, kuombewa kwa imani kwa kudhani ni mapepo.

Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Patience Njenje, aliyasema hayo jana wakati wa kutoa elimu kwa umma eneo la Manzese, Dar es Salaam, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kifafa Kuniani.

Dk. Njenje, alieleza kuwa baadhi ya wagonjwa wa Kifafa wana imani potofu, kwamba ugonjwa huo ni wa kuambukiza, kurogwa au nguvu za giza na kwamba sababu ya ugonjwa kitaalumu ziko wazi ambazo zimefanyiwa utafiti.

Habari hii kwa kina iko kwenye gazeti la TanzaniaDaima la leo Jumanne Februari 11. Pata nakala yako kwa habari zaidi

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *