AJALI, Abiria 29 Basi la Saibaba wanusurika vifo

Habari Hot

PWANI, TANZANIA

ABIRIA zaidi ya 29 wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori lililobeba kokoto, katika eneo la Kongowe wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo alisema kwamba tukio hilo limetokea jana saa 1 asubuhi katika barabara ya Morogoro.

Kamanda Nyigesa alisema, lori hilo lenye namba za usajili T 641 DPJ na tela lenye namba T 643 DPJ, liliokuwa katika mwendokasi, lilikutana uso kwa uso na basi la abiria la Saibaba lenye namba T 779 ARW, lililokuwa likiendeshwa na Richard Wilfred.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, aliyekuwa akiendesha kwa mwendokasi katika eneo lisiloruhusiwa na kusababisha ajali hiyo.

Kamanda huyo alisema, kuwa basi hilo lilitokea Sumbawanga kuelekea jijini Dar es Salaam.

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *