UTAFITI; Watu 400 kati ya 2,000 wagundulika na Virusi vya Homa ya Ini

Habari Hot

DAR ES SALAAM, TANZANIA

WATU 2,000 waliofanyiwa utafiti wa maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini, 400 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, ambao ni sawa na asilimia 40, wakiwa hatarini kupata Saratani ya Ini.

Aidha, imebainika kuwa asilimia 90ya wanaopata maambukizi hayo ni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. John Rwegesha, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, katika kongamano lililokutanisha Wataalamu wa Afya kujadili maendeleo ya Mradi wa Tiba ya Virusi vyo Homa ya Ini, ulioanzishwa na MNH miaka minne iliyopita.

Dk. Rwegasha alisema, mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2021, lengo likiwa ni kubaini kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo, ambao ulienea kwa kiasi kikubwa nchini kutokana na kukosa tiba pamoja na vitendanishi kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema mradi huo ambao umefadhiliwa na Marekani, una vifaa vya kufanya vipimo na imefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kuwafanyia tathmini watu 2,000 ambao ndio lengo la mradi huo.

Alisema wanaopata maambuziki hayo ni kuanzia umri wa miaka 30 hadi 40 na kwamba maambukizi huweza kukaa mwilini kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya dalili na kwamba kati ya watu 100, watu watano wameathirika na maambukizi hayo kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS).

BIMA BANNER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *