Maalim Seif Sharif Hamad aachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Polisi Pemba

KASKAZINI PEMBA, ZANZIBAR MSHAURI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, Salim Bimani, ambao waliitikia wito wa kufika ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Kaskazini Pemba, leo Januari 14, wameachiwa kwa dhamana. Baada ya kuachiwa kwa […]

Continue Reading

SIASA CHAFU; M/kiti, Mtendaji Kata washusha, kuchana Bendera za Vyama vya upinzani Kilwa

KILWA, TANZANIA UONGOZI wa Serikali ya Kijiji na Kata ya Songo-Mnara, wilayani Kilwa mkoani Lindi, umedaiwa kushusha na kuchana Bendera za Chama cha ACT-Wazalendo, kwa kile kilichoelezwa maandalizi ya kupokea ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi, katani humo. Tukio la ushushaji na uchanaji bendera, unadaiwa kufanywa Januari 7 katika Kata ya […]

Continue Reading

UBAKAJI; Mtoto wa miaka 10 anajisiwa, auawa na mwili wake kutelekezwa msituni

KATAVI, TANZANIA KIZA kinene cha mauaji na matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kimeendelea kuufunika mwaka mpyaa wa 2020, hii ni baada muendelezo wa kuripotiwa kwa matukio, kunajisiwa na kuuawa kwa mwanafuzni wa darasa la nne, Shule ya Msingi Katisunga, Mpanda mkoani Katavi. Taarifa za tukio hilo zinapasha kuwa, mwanafunzi huyo mwenye umri wa […]

Continue Reading

HATI ZA ARDHI ‘zamtokea puani’ Mkuu wa Idara Manispaa ya Mtwara Mikindani

MTWARA, TANZANIA NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula, ameagizwa kuondolewa kazini kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa yam TWARA Mikindani mkoani Mtwara, Mariam Kimoro, baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa Sekta ya Ardhi katika manispaa hiyo. Uamuzi wa Naibu Waziri Mabula kumvua wadhifa huo Kimoro, kuwa Mkuu […]

Continue Reading

AHUKUMIWA kifungo cha maisha jela kwa kubaka mtoto wa miaka mitatu

BUNDA, TANZANIA MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imemuhukumu kifungo cha maisha jela, Masatu Mjarifu (35), ambaye ni Mvuvi na mkazi wa Kijiji cha Mahyolo wilayani humo, baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka mitatu. Hukumu hiyo ilitolewa jana naa Hakimu Mkazi Mwandamzi wa Mahakama hiyo, Jackline Rugemalira, baada […]

Continue Reading

Matukio ya kingono na ukatili wa kijinsia Iringa yaongezeka

IRINGA, TANZANIA VITENDO vya Ukatili wa Kingono, ambalo ni tatizo kubwa miongoni mwa matatizo yanayowakabili watoto katika malezi na makuzi yao mkoani Iringa, vimeelezwa kuongezeka na kufikia matukio 404 katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2019. Hayo, yamebainika mkoani Iringa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee […]

Continue Reading

Serikali yavunja mkataba na NICOL, Waziri Mpina atoa maagizo mazito

DODOMA, TANZANIA SERIKALI imevunja mkataba na Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL), wa uendeshaji wa kiwanda cha kuchinjia nyama cha Dodoma, sababu kuu ikitajwa kuwa ji udanganyifu kwenye u]mkataba huo ambao umelisababishia taifa hasara inayokadiriwa kufikia Sh. Bilioni 9.7. Akizungumza jijini hapa jana, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, amesema tangu waikabidhi Kampuni ya […]

Continue Reading

Mtoto afariki dunia na watu wengine 30 walazwa baada ya kula mzoga wa nguruwe

RUKWA, TANZANIA MTOTO aliyetajwa kwa jina la Mareni Namsukuma mwenye umri wa miaka 7, amefariki dunia na wengine 30 wakazi wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wanaendelea kupatiwa matibabu baada ya kula nyama ya mzoga wa Nguruwe Imeelezwa kuwa, mmoja kati ya wanakijiji mwenzao, aliwauzia nyama ya Nguruwe ambaye alikuwa amekufa bila kujua kilichomuua, ambako […]

Continue Reading

Rais Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) asimamishwa masomo UDSM kwa muda usiojulikana

DAR ES SALAAM, TANZANIA RAIS wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO), Hamis Mussa Hamis, amesimamishwa masomo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na tayari amepewa barua ya kuondoka chuoni hapo kwa muda usiojulikana, iliyosainiwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. William Anangisye. Kufungiwa kwa Hamis kumekuja baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, […]

Continue Reading

Waziri Mbarawa: Aliyejenga ofisi hii kwa Sh. Mil. 100 akamatwe!

MBEYA, TANZANIA HUYU Mkandarasi Mungu anamuona aisee, daaah! Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, ameamuru kukamatwa kwa Alistides Kanyomo, Mhandisi na Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwakaleli uliopo Halmashauri ya Busokelo mkoani Mbeya. Mradi huo unatekelezwa na Kampuni ya Mbesso Construction Ltd ya Dar es Salaam, ambako agizo la Waziri Mbarawa, limetokana na kutoridhishwa […]

Continue Reading